Kinhuwala
lugha ya asili ya Australia iliyotoweka / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kinhuwala kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wanhuwala katika jimbo la Australia Magharibi. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kinhuwala ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kinhuwala kiko katika kundi la Kipama-Nyungan cha Kusini-Magharibi.