Kingarla
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kingarla ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wangarla katika jimbo la Australia Magharibi. Mwaka wa 2012, kulikuwa na wasemaji wa Kingarla 18 tu, na lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kingarla kiko katika kundi la Kipama-Nyungan cha Kusini-Magharibi.