Kingarinman
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kingarinman ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wangarinman katika jimbo la Northern Territory. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kingarinman 375 (pamoja na wasemaji wa lahaja ya Kibilinara), na lugha imo hatarini mwa kutoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kingarinman kiko katika kundi la Kipama-Nyungan cha Kusini-Magharibi.