Kingarigu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kingarigu ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wangarigu katika jimbo la New South Wales. Mwaka wa 2004, idadi ya wasemaji wa Kingarigu ilihesabiwa kuwa watu watano tu, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kingarigu kiko katika kundi la Kiyuin.