Kingardi
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kingardi ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wangardi katika jimbo la Northern Territory. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kingardi 14 tu, na lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kingardi kiko katika kundi la Kipama-Nyungan cha Kusini-Magharibi.