Kingamini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kingamini kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wangamini katika jimbo la Australia Kusini. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kingamini ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kingamini kiko katika kundi la Kikarniki.