Kinari-Nari
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kinari-Nari kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wanari-Nari katika jimbo la New South Wales. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea Kinari-Nari, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kinari-Nari kiko katika kundi la Kikulin.