Kimullukmulluk
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kimullukmulluk ni lugha ya Kidaly nchini Australia inayozungumzwa na Wamullukmulluk katika jimbo la Northern Territory. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kimullukmulluk 33 tu, yaani lugha imekaribia kutoweka hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimullukmulluk kiko katika kundi la Kimalagmalag.