Kimudburra
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kimudburra (au Kimudbura) ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wamudburra katika jimbo la Northern Territory. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kimudburra 47 tu, na lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimudburra kiko katika kundi la Kipama-Nyungan cha Kusini-Magharibi.