Kiminang
lugha ya asili ya Australia iliyotoweka / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiminang (au Kimirnong) kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Waminang katika jimbo la Australia Magharibi. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kiminang ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiminang kiko katika kundi la Kipama-Nyungan cha Kusini-Magharibi. Wengine hukiangalia kuwa lahaja ya Kinyunga.