Kimartu-Wangka
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kimartu-Wangka ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wamartu-Wangka katika jimbo la Australia Magharibi. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kimartu-Wangka 880. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimartu-Wangka kiko katika kundi la Kipama-Nyungan cha Kusini-Magharibi.