Kimarkesa-Kusini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kimarkesa ya Kusini ni lugha ya Kiaustronesia nchini Polinesia ya Kifaransa inayozungumzwa na Wamarkesa, hasa kwenye visiwa vya Hiva Oa, Tahuata na Fatu Hiva. Mwaka wa 2007 idadi ya wasemaji wa Kimarkesa ya Kusini imehesabiwa kuwa watu 2700. Wamarkesa ya Kusini wengi wanatumia lugha ya Kitahiti badala ya lugha yao ya asili, yaani lugha ya Kimarkesa ya Kusini iko hatarini mwa kutoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimarkesa ya Kusini iko katika kundi la Kioseaniki.