Kimarithiel
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kimarithiel ni lugha ya Kidaly nchini Australia inayozungumzwa na Wamarithiel katika jimbo la Northern Territory. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kimarithiel 15 tu, yaani lugha imekaribia kutoweka hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimarithiel kiko katika kundi la Kibringen.