Kimaringarr
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kimaringarr ni lugha ya Kidaly nchini Australia inayozungumzwa na Wamaringarr katika jimbo la Northern Territory. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kimaringarr sita tu, yaani lugha imekaribia kutoweka hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimaringarr kiko katika kundi la Kibringen.