Kimarimanindji
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kimarimanindji ni lugha ya Kidaly nchini Australia inayozungumzwa na Wamarimanindji katika jimbo la Northern Territory. Mwaka wa 2005, kulikuwa na wasemaji wa Kimarimanindji kumi tu, yaani lugha imekaribia kutoweka hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimarimanindji kiko katika kundi la Kibringen.