Kimangala
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kimangala (au Kimangarla) ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wamangala katika jimbo la Australia Magharibi. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kimangala 61 tu, na lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimangala kiko katika kundi la Kipama-Nyungan cha Kusini-Magharibi.