![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/1/19/WIKITONGUES-_Omar_speaking_Mandinka.webm/640px--WIKITONGUES-_Omar_speaking_Mandinka.webm.jpg&w=640&q=50)
Kimandinka
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kimandinka ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Senegal, Gambia na Guinea-Bisau inayozungumzwa na Wamandinka. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kimandinka imehesabiwa kuwa watu 669,000 nchini Senegal, 510,000 nchini Gambia, na 167,000 nchini Guinea-Bisau. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimandinka iko katika kundi la Kimande.