Kimalyangapa
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kimalyangapa kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wamalyangapa katika jimbo la New South Wales. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea Kimalyangapa, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimalyangapa kiko katika kundi la Kiyarli.