Kimadhi-Madhi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kimadhi-Madhi (au Kimuthimuthi) kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wamadhi-Madhi katika jimbo la New South Wales. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea Kimadhi-Madhi, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimadhi-Madhi kiko katika kundi la Kikulin.