Kilardil
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kilardil ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Walardil katika jimbo la Queensland. Katika sensa ya mwaka wa 2006, idadi ya wasemaji wa Kilardil ilikuwa watu 54 tu, yaani lugha imekaribia kutoweka hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kilardil kiko katika kundi lake lenyewe la Kilardil.