Kikurrama
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kikurrama ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wakurrama katika jimbo la Australia Magharibi. Mwaka wa 2005, kulikuwa na wasemaji wa Kikurrama kumi tu, na lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikurrama kiko katika kundi la Kipama-Nyungan cha Kusini-Magharibi.