Kikurnai
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kikurnai (pia Kiganai) ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wakurnai katika jimbo la Victoria. Mwaka wa 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kikurnai 26 tu, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikurnai kiko katika kundi la Kiganaiki.