Kikungardutyi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kikungardutyi kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wakungardutyi katika jimbo la Victoria. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kikungardutyi ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikungardutyi kiko katika kundi la Kikarniki.