Kikumbainggar
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kikumbainggar (au Kigumbaynggir) ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wakumbainggar katika jimbo la New South Wales. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kikumbainggar 42 tu, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikumbainggar kiko katika kundi la Kigumbaynggiriki.