Kikuku-Yalanji
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kikuku-Yalanji ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wakuku katika jimbo la Queensland. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kikuku-Yalanji 360, na lugha imo hatarini mwa kutoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikuku-Yalanji kiko katika kundi la Kiyalandyiki.