Kikuku-Uwanh
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kikuku-Uwanh ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wakuku katika jimbo la Queensland. Mwaka wa 1981, kulikuwa na wasemaji wa Kikuku-Uwanh 40 tu, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikuku-Uwanh kiko katika kundi la Kipaman.