Kikuku-Muminh
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kikuku-Muminh ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wakuku katika jimbo la Queensland. Mwaka wa 2005, kulikuwa na wasemaji wa Kikuku-Muminh 20 tu, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikuku-Muminh kiko katika kundi la Kipaman.