Kikoongo
lugha inayozungumzwa na Wakongo wanaoishi Angola na Kongo hizo mbili / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kikoongo (pia: Kikongo) ni lugha ya Kibantu hasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako inahesabiwa kati ya lugha 4 za kitaifa. Kinazungumzwa na Wakoongo. Idadi ya wasemaji wa Kikoongo kama lugha ya kwanza katika Jamhuri imehesabiwa kuwa watu milioni tatu; pamoja na hayo kuna watu milioni tano ambao huongea Kikoongo kama lugha ya pili. Tena kuna wasemaji wa Kikoongo milioni moja nchini Angola na milioni moja nchini Jamhuri ya Kongo. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kikoongo iko katika kundi la H10.