Kikaruwali
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kikaruwali (pia Kimithaka) kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wakaruwali katika jimbo la Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kikaruwali ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikaruwali kiko katika kundi la Kikarniki.