Kikarniki cha Mashariki
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kikarniki cha Mashariki (pia Kingura) kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wakarniki katika majimbo ya New South Wales na Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kikarniki cha Mashariki ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikarniki cha Mashariki kiko katika kundi la Kikarniki.