Kikarenggapa
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kikarenggapa kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wakarenggapa katika majimbo ya New South Wales na Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kikarenggapa ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikarenggapa kiko katika kundi la Kikarniki.