Kikaradjeri
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kikaradjeri (au Kigaradjari) ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wakaradjeri katika jimbo la Australia Magharibi. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kikaradjeri 26 tu, na lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikaradjeri kiko katika kundi la Kipama-Nyungan cha Kusini-Magharibi.