Kiiu-Mien
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiiu-Mien ni lugha ya Kihmong-Mien nchini Vietnam, Uchina, Uthai na Laos inayozungumzwa na Wamien. Mwaka wa 1999 idadi ya wasemaji wa Kiiu-Mien imehesabiwa kuwa watu 350,000 nchini Vietnam na 40,000 nchini Uthai. Pia kuna wasemaji 383,000 nchini Uchina (1995) na 20,300 nchini Laos (2000). Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kiiu-Mien iko katika kundi la Kimian-Jin.