Kiilocano
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiilocano ni lugha ya Kiaustronesia nchini Ufilipino inayozungumzwa na Wailocano. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kiilocano imehesabiwa kuwa watu 6,920,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiilocano iko katika kundi la Kifilipino.