Kiguwa
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiguwa kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Waguwa katika jimbo la Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kiguwa ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiguwa kiko katika kundi la Kimariki.