Kigurinji
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kigurinji ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wagurinji katika jimbo la Northern Territory. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kigurinji 590, hata hivyo lugha imo hatarini mwa kutoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kigurinji kiko katika kundi la Kipama-Nyungan cha Kusini-Magharibi.