Kigureng-Gureng
lugha ya asili ya Australia iliyotoweka / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kigureng-Gureng kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wagureng-Gureng katika jimbo la Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea Kigureng-Gureng, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kigureng-Gureng kiko katika kundi la Kiwaka-Kabiki.