Kigurdjar
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kigurdjar ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wagurdjar katika jimbo la Queensland. Mwaka wa 2007, kulikuwa na msemaji mmoja wa Kigurdjar tu, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kigurdjar kiko katika kundi la Kipaman.