Kigungabula
lugha ya asili ya Australia iliyotoweka / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kigungabula kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wagungabula katika jimbo la Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kigungabula ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kigungabula kiko katika kundi la Kimariki.