Kigunditjmara
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kigunditjmara kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wagunditjmara katika jimbo la Victoria. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea Kigunditjmara, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kigunditjmara kiko katika kundi la Kibunganditj.