Kigugubera
lugha ya asili ya Australia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kigugubera (au Kikoko-Bera) ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wagugubera katika jimbo la Queensland. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kigugubera 100, na lugha imo hatarini mwa kutoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kigugubera kiko katika kundi la Kipama cha Kusini-Magharibi.