Kigugu-Warra
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kigugu-Warra kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wagugu-Warra katika jimbo la Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kigugu-Warra imetoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kigugu-Warra kiko katika kundi la Kipaman.