Kigaringbal
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kigaringbal kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wagaringbal katika jimbo la Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kigaringbal ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kigaringbal kiko katika kundi la Kimariki.