Kigamilaraay
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kigamilaraay ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wagamilaraay katika majimbo ya Queensland na New South Wales. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kigamilaraay 35 tu, tena wote walichanganya lugha yao ya asili na Kiingereza. Kwa hiyo lugha kama lugha halisi imeshatoweka. Hata hivyo Kigamilaraay hufundishwa katika shule kadhaa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kigamilaraay kiko katika kundi la Kiwiradhuriki.