Kiewe
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiewe ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Ghana na Togo inayozungumzwa na Waewe. Mwaka wa 2003 idadi ya wasemaji wa Kiewe nchini Ghana imehesabiwa kuwa watu 2,250,000. Pia kuna wasemaji 862,000 nchini Togo. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiewe iko katika kundi la Kikwa.