Kidyangadi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kidyangadi (au Kidhanggati) ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wadyangadi katika jimbo la New South Wales. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kidyangadi watano tu, lakini hao ni matokeo ya mradi wa kufufua lugha ya Kidyangadi. Maana yake, lugha iliachwa kuzungumzwa wakati wa miaka ya 1960; halafu mwaka 2000 shule ikaanzishwa kwa ajili ya kufundisha lugha ya Kidyangadi tena. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kidyangadi kiko katika kundi la Kiyidiny.