Kigelao Nyeupe
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kigelao Nyeupe (pia Kiduoluo) ni lugha ya Kitai-Kadai nchini Uchina na Vietnam inayozungumzwa na Wagelao. Mwaka wa 1987 idadi ya wasemaji wa Kigelao Nyeupe nchini Uchina imehesabiwa kuwa watu 1200. Pia kuna wasemaji 20 tu nchini Vietnam (2002). Lugha ya Kigelao Nyeupe imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kigelao Nyeupe iko katika kundi la Kikra.