Kidjadjawurrung
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kidjadjawurrung kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wadjadjawurrung katika jimbo la Victoria. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kidjadjawurrung ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kidjadjawurrung kiko katika kundi la Kikulin.