Kidhungaloo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kidhungaloo (au Kidungaloo) kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wadhungaloo katika jimbo la Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kidhungaloo ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kidhungaloo kiko katika kundi la Kimariki.