Kidharuk
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kidharuk (au Kidharug) kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wadharuk katika jimbo la New South Wales karibu na mji wa Sydney. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kidharuk ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kidharuk kiko katika kundi la Kiyora.